Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Nchini Nepal, warakati za uokoaji zikiendelea kuna hofu inayotanda juu ya uwezekano wa mafuriko mengine zaidi , mamia wamepoteza maisha , wengine kuokolewa na miundombinu kkusambaratishwa UN inafanya kila liwezekanalo kusaidia -Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa katab awa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa, UNCCD COP17, umehitimishwa hii leo mjini Ulaanbaatar, Mongolia, baada ya wiki mbili za majadiliano kuhusu uharibifu wa ardhi, kuenea kwa jangwa na ukame -Na Katika Kaunti za Garissa na Mandera nchin
Na sasa ni wasaa wa kujifunza Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno Kirobezo. Hili linahusu wale wanaopenda kupitapita maeneo ya watu kuvizia mlo.
Leo jaridani kuna Mada kwa Kina inakupeleka Uganda kumulika Siku ya Ziwa duniani hususan Ziwa Albert. Lakini pia kuna Muhtasari ukiwasilishwa na Leah Mushi akiangazia kumalizika kwa mlipuko wa Ebola, Uganda; Kauli ya Katibu Mkuu wa UM kuhusu maambukizi ya Ebola nchini DR Congo na kisha chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini. Jifunze Kiswahili leo inabisha hodi nchini Burundi kwa Mwenyekiti wa CHAWARUNDI Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
Leo mada yetu kwa kina inaangazia mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa UNCCD COP17 unaofanyika huko mjini Ulaanbaatar, Mongolia kuanzia tarehe 17 mpaka 28 mwezi huu. Mwenzangu Leah Mushi wa idhaa hii amezungumza na wadau wanaohudhuria mkutano huo, wa kwanza anaanza kwa kujitambulisha.
UN na ICRC watoa wito mpya wa kanuni kuhusu silaha zinazojiendesha zenyewe. Mageuzi ya Kilimo ya Malawi: Mwanzo mpya kwa wakulima wadogo. Vijana wa Yambio Sudan Kusini wataka elimu, usalama na nafasi zaidi katika uamuzi.
Siku 100 tangu Ebola kutangazwa nchini DRC hali inazidi kuwa mbaya. Pamoja na kuchukua hatua WHO yaonya kuhusu kuongezeka kwa wagonjwa wa mpox Guinea-Bissau. Ufadhili mpya wa dola milioni 22 za marekani kwa elimu ya watoto walioathiriwa na mgogoro Sudan.
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nduha anakuletea -Julien Harneis, Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ebola amesema nchini DRC “Katika miezi mitatu iliyopita watu 2,500 wamekufa na nusu yao wamekufa katika kipindi cha siku tatu zilizopita na mlipuko unaendelea kusambaa zaidi, hivi sasa umesambaa katika eneo lenye ukubwa sawa na nchi ya Ufaransa.” -Hali ya ukosefu wa fedha ni mbaya pia nchini Somalia ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema kuwa kupunguzwa kwa ufadhili wa kibinadamu nchini Somalia kumesababisha kufungwa kwa vituo 205 vya
Tume ya UN: Uchaguzi Sudan Kusini usigeuke kuwa uwanja mwingine wa mapigano WFP yaongeza operesheni za msaada kwa manusra wa teteko la ardhi Colombia Umoja wa Mataifa na Sudan Kusini waimarisha maandalizi dhidi ya Ebola
Leo katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataofa Flora Nducha anakuletea --Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wahudumu wa Kibinadamu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kuwalinda wahudumu wa kibinadamu wanaotoa msaada wa kuokoa maisha katika maeneo yenye migogoro -Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura (OCHA) iliyotolewa leo katika kuadhimisha hii imeonya kwamba wahudumu 907 wa kibinadamu walikumbwa na vitendo vya ukatili mwaka jana, wakati wakitekeleza kazi zao za kuokoa maisha katika maeneo
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KARAKARA"
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Leo WHO imefanya mkutano wa pili wa kamati ya dharura ya kanuni za afya za Kimataifa mjini Geneva Uswisi kutathmini kuhusu mlipuko wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. -WHO pia imezungumza na waandshi wa habari DRC katika jitihada za kupambana na Ebola na pia kuhakikisha jamii inashirikishwa ipasavyo ikiwemo waendesha pikipiki au boda boda -Ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF, imeonesha kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika muongo mmoja uliopita, vituo vi
Zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi 650,000 nchini Sudan Kusini wako katika hatari ya kupoteza msaada muhimu wa chakula na lishe kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, na lile linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR zimeonya. Kupunguzwa kwa msaada kunaweza kuwaathiri wakimbizi 240,000 ndani ya wiki chache, wakati nchi hiyo yenyewe ikikabiliwa na ongezeko la tatizo la njaa. Feissal Kirwa na taariifa zaidi (TAARIFA YA FEISSAL KIRWA) Nattss….. Katika makazi ya wakimbizi ya Wedweil nchini Sudan Kusini, akina mama na watoto wanasubiri
Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) tangu mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaimarisha sekta ya mwani, kwa kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuongeza uzalishaji, tija na kipato. Miongoni mwa walionufaika zaidi ni vikundi vya wanawake, ambavyo vimejengewa uwezo kuhusu mbinu bora za uzalishaji, uanikaji na uhifadhi wa mwani, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi anatuletea taarifa inayomhusu mnufaika mmoja wa mafunzo hayo. (Taarifa ya Assumpta Massoi) Jumla
Zoezi la siku tano la utoaji chanjo dhidi ya polio limekamilika katika mkoa wa Banadir nchini Somalia, likiwafikia watoto zaidi ya 122,000 walio chini ya umri wa miaka mitano. Kampeni hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora Nducha. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Kampeni hiyo imetekelezwa katika wilaya za Daynile, Garasbaley na Kahda, ambako kuna familia nyingi zilizolazimika kuyakimbia makazi yao na ambazo imekuwa vigumu kuwafikia watoto wao katika kampeni zilizopita. Kwa muda wa miezi mitatu, Wiz
Karibu usikilize jarida la habari za UN ambalo leo habari zake zote zimetoka barani Afrika. Utasikia kuhusu juhudi za kutoa chanjo wa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 huko nchini Somalia. Utasikia namna FAO inavyowasaidia wananchi huko Zanzibar kuongeza ubora wa zao la Mwani. Na mwisho utasikia ufinyu wa bajeti unavyoathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini.
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo utasikia mahojiano na kijana kutoka nchini Kenya Feisal Kirwa aliyekuwa akishiriki mafunzo kwa Vitendo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa muda wa miezi sita na sasa amehitimu mafunzo hayo. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari.
Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Harakati za kutokomeza Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zinakumbwa na mkwamo kwani wananchi wamesema wanahitaji sio tu matibabu dhidi ya ugonjwa huo, bali pia maji, chakula, matibabu ya malaria, chanjo na huduma za afya uzazi, mama na mtoto. -hirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya kuhusu ubora wa maji ya kunywa, likizitaka nchi kuimarisha kanuni, ufuatiliaji na usimamizi wa hatari zozote zinazoweza kujitokeza . Licha ya maendeleo ya
Katika Jarida la habari hii leo Flora Nducha anakuletea -Leo ni Siku ya vijana Duniani Umoja wa Mataifa wasisitiza umuhimu wa kuwasikiliza, kuwapa fursa na kuwasaidia vijana kuchangia na kushamiri katika jamii -Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kuhusu ajira kwa kundi la vijana inasema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana duniani umeongezeka, huku ukuaji dhaifu wa uchumi na upungufu wa nafasi mpya za kazi ukiwaweka vijana katika mazingira magumu ya kuingia katika soko la ajira. -Katika mada kwa kina utamsikia kijana kutoka Tanzania Zephania Opiyo aliyepata fursa ya mafu
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Feissal Kirwa anakuletea -Idadi ya vifo na majeruhi kufuatia tetemeko la ardhi nchini Colombia inaongezeka huku Umoja wa Mataifa ukianza kuwasilisha msaada muhimu kwa waathirika na kuwa tayari kusaidia kwa kila hali -Nchini Tanzania serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF inahakikisha kila mtoto anasajiliwa pindi anapozaliwa -Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana itakayoadhimishwa kesho Agosti 12 leo utasikia sauti za vijana mbalimbali wakigusia ajira, elimu na maisha kw